Tunaomba Uwepo Wako Uende Nasi Lyrics

Tunaomba Uwepo Wako Uende Nasi Lyrics By Reuben Kigame, Sifa Voices. Tunaomba uwepo wako uende nasi Ewe bwana wa majeshi tusikie Kama uendi nasi hatutaki kutoka hapa Hatuwezi peke yetu enda nasi Tu watu wa shingo ngumu tusamehe Hatufai mbele zako turehemu.

Tunaomba Uwepo Wako Uende Nasi Lyrics

Tunaomba uwepo wako uende nasi
Ewe bwana wa majeshi tusikie
Kama uendi nasi hatutaki kutoka hapa
Hatuwezi peke yetu enda nasi

Tu watu wa shingo ngumu tusamehe
Hatufai mbele zako turehemu
Tusafishe baba tuonyeshe uso wako
Twahitaji neema yako enda nasi

Tutavua mapambo yetu
Vitu vyote vya dhamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi

Tunaomba utuonyeshe njia zako Kwa maan umetuita kwa jina lako
Twalilia e bwana utukufu na uso wako
Bila wewe tutashindwa enda nasi

Tutavua mapambo yetu
Vitu vyote vya dhamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi

Ndugu na dada yangu tafadhali usijaribu kuyamudu maisha bila yake bwana utashindwa
Yafaa tufike mahali ambapo musa alimlilia bwana na kutafuta uso wake
Na kusema bwana tafadhali enda nasi enda nasi twakuhitaji.

Tutavua mapambo yetu
Vitu vyote vya dhamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi X2

Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi X2

Sigma Male Rules Song Lyrics