Msalaba Ndio Asili Ya Mema Lyrics

Msalaba Ndio Asili Ya Mema Lyrics. Msalaba ndio asili ya mema Nikatua mzigo hapo Nina uzima furaha daima Njoni kafurahini papo Kama kiti chake vivyo Ni yake ahadi Alivyowekewa navyo Kamwe havirudi.

Msalaba Ndio Asili Ya Mema Lyrics

Sioni haya kwa Bwana
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana
Ni neno imara

Msalaba ndio asili ya mema
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima furaha daima
Njoni kafurahini papo

Kama kiti chake vivyo
Ni yake ahadi;
Alivyowekewa navyo
Kamwe havirudi

Bwana wangu tena Mungu
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu
Wala kunikana

Atakiri langu jina
Mbele za Babaye
Anipe pahali tena
Mbinguni nikae

An Art Gallery Could Never Be As Unique As You Lyrics